MBWAWA COMMUNITY DEVELOPMENT ASSOCIATION
VIONGOZI NA WANACHAMA WA MBWAWA COMMUNITY DEVELOPMENT WAKUTANA LEO. Dar es Salaam. Wanajumuiya ya Mbwawa Development Community leo 11/10/2020 wamekutana na kufanya kikao cha kwanza katika ofisi ya taasisi ya JAI iliyopo Kinondoni Hospitali. Kikao hicho kimejumuisha viongozi na wajumbe kilianza saa 03:00 asubuhi na kuisha saa 06:00 mchana. Katibu wa jumuiya hiyo ndugu Yassin Ngupili ameeleza kuwa lengo la kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ni kusaidia maendeleo katika jamii hususani wana Mbwawa. Pia ameongezea kuwa maendeleo hayo hayatanufaisha wanambwawa tu peke yake bali yatanufaisha kata, wilaya, mkoa na taifa kwa ujumla. “Sasa ni wakati wa kuisajili jumuiya yetu haraka iwezekanavyo ili itambulike kisheria. Na tuanze upya kuwasajili wanachama hai. Pia tunawakaribisha wanambwawa wapenda maendeleo wanaotaka kujiunga nasi” Amesema Mwenyekiti bwana Hamis Mmanga. Hata hivyo Mlezi wa jumuiya hiyo Dr. Pazi Mwinyimvua amebainisha kwamba vipaumbele vya jumuiy...