Tarehe 11/04/2021
AFISA HABARI WA MCDA AKUTANA NA DIWANI WA KATA YA MBWAWA. MISWE. Afisa habari wa taasisi ya Mbwawa Community Development Association (MCDA) ndugu Maulid Rashid Lijonjo, juzi amekutana na kufanya mazungumzo na Mh. Diwani wa kata ya Mbwawa Judith Bernald Mruge nyumbani kwake kijijini Miswe. Afisa habari huyo aliweza kuitambulisha taasisi ya MCDA kwa Mh. Diwani. Diwani Judith Bernald Mruge amepongeza juhudi zilizofanywa na viongozi wa taasisi hiyo, ikiwemo kufanya kikao cha kutunga katiba ya taasisi na kuanza mchakato wa usajili. Aidha Diwani amewataka viongozi wa MCDA kukutakana na wenyeviti wote wa Miswe na Mbwawa ili kurahisisha usajili wa taasisi hiyo. "Taasisi au chama ni lazima kitambulike kuanzia ngazi ya kijiji. Ni lazima mkae kikao na wenyeviti wote wa Miswe na Mbwawa, na wao watakaa kikao na mimi, na mimi nitakaa kikao na mtendaji kata, kisha jambo lenu nitalipeleka moja kwa moja huko halmashauri" . Amesema Mh.Judith Bernald Mruge. Kwa upande wao viongozi wa ta...