Machapisho

Tarehe 11/04/2021

  AFISA HABARI WA MCDA AKUTANA NA DIWANI WA KATA YA MBWAWA. MISWE. Afisa habari wa taasisi ya Mbwawa Community Development Association (MCDA) ndugu Maulid Rashid Lijonjo, juzi  amekutana na kufanya mazungumzo na Mh. Diwani wa kata ya Mbwawa Judith Bernald Mruge nyumbani kwake kijijini Miswe. Afisa habari huyo aliweza kuitambulisha taasisi ya MCDA kwa Mh. Diwani. Diwani Judith Bernald Mruge  amepongeza juhudi zilizofanywa na viongozi wa taasisi hiyo, ikiwemo kufanya kikao cha kutunga katiba ya taasisi na kuanza mchakato wa usajili. Aidha Diwani amewataka viongozi wa MCDA kukutakana na wenyeviti wote wa Miswe na Mbwawa ili kurahisisha usajili wa taasisi hiyo. "Taasisi au chama ni lazima kitambulike kuanzia ngazi ya kijiji. Ni lazima mkae kikao na wenyeviti wote wa Miswe na Mbwawa, na wao watakaa kikao na mimi, na mimi nitakaa kikao na mtendaji kata, kisha jambo lenu nitalipeleka moja kwa moja huko halmashauri" . Amesema Mh.Judith Bernald Mruge. Kwa upande wao viongozi wa ta...
 UTAMBULISHO WA UONGOZI

MBWAWA COMMUNITY DEVELOPMENT ASSOCIATION

 VIONGOZI NA WANACHAMA WA MBWAWA   COMMUNITY DEVELOPMENT WAKUTANA LEO. Dar es Salaam. Wanajumuiya ya Mbwawa Development Community leo 11/10/2020 wamekutana na kufanya kikao cha kwanza katika ofisi ya taasisi ya JAI iliyopo  Kinondoni Hospitali.  Kikao hicho kimejumuisha viongozi na wajumbe kilianza saa 03:00 asubuhi na kuisha saa 06:00 mchana.  Katibu wa jumuiya hiyo ndugu Yassin Ngupili ameeleza kuwa lengo la kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ni kusaidia maendeleo katika jamii hususani wana Mbwawa. Pia ameongezea kuwa maendeleo hayo hayatanufaisha wanambwawa tu peke yake bali yatanufaisha kata, wilaya, mkoa na taifa kwa ujumla.  “Sasa ni wakati wa kuisajili jumuiya yetu haraka iwezekanavyo ili itambulike kisheria. Na tuanze upya kuwasajili wanachama hai. Pia tunawakaribisha wanambwawa wapenda maendeleo wanaotaka kujiunga nasi” Amesema Mwenyekiti bwana Hamis Mmanga. Hata hivyo Mlezi wa jumuiya hiyo Dr. Pazi Mwinyimvua amebainisha kwamba vipaumbele vya jumuiy...