Tarehe 11/04/2021

 


AFISA HABARI WA MCDA AKUTANA NA DIWANI WA KATA YA MBWAWA.


MISWE. Afisa habari wa taasisi ya Mbwawa Community Development Association (MCDA) ndugu Maulid Rashid Lijonjo, juzi  amekutana na kufanya mazungumzo na Mh. Diwani wa kata ya Mbwawa Judith Bernald Mruge nyumbani kwake kijijini Miswe. Afisa habari huyo aliweza kuitambulisha taasisi ya MCDA kwa Mh. Diwani.


Diwani Judith Bernald Mruge  amepongeza juhudi zilizofanywa na viongozi wa taasisi hiyo, ikiwemo kufanya kikao cha kutunga katiba ya taasisi na kuanza mchakato wa usajili.


Aidha Diwani amewataka viongozi wa MCDA kukutakana na wenyeviti wote wa Miswe na Mbwawa ili kurahisisha usajili wa taasisi hiyo. "Taasisi au chama ni lazima kitambulike kuanzia ngazi ya kijiji. Ni lazima mkae kikao na wenyeviti wote wa Miswe na Mbwawa, na wao watakaa kikao na mimi, na mimi nitakaa kikao na mtendaji kata, kisha jambo lenu nitalipeleka moja kwa moja huko halmashauri". Amesema Mh.Judith Bernald Mruge.


Kwa upande wao viongozi wa taasisi ya MCDA wamefarijika sana kuona Diwani ameipokea taasisi hiyo kwa mikono miwili. Na wameahidi kushirikiana na  Diwani huyo katika shughuli za kimaendeleo za kuijenga Mbwawa mpya yenye maendeleo. "Ni furaha iliyoje kupata kiongozi kama huyu imara, shupavu, mpenda maendeleo na mwenye uchungu na kata yetu ya mbwawa". Alisema Mwenyekiti wa MCDA ndugu Khamis Mmanga.


Hata hivyo Mh.Judith Bernald Mruge aliezea fursa zilizopo katika kata yake ikiwemo mikopo ya halmashauri ambapo ameshauri ndani ya wanachama wa MCDA viuundwe vikundi vya watu 7  au 10 ili kupata pesa za halmshauri pesa ambazo zitatumika kuanzisha miradi mbalimbali ili kuleta maendeleo kwa jamii. Aidha amefurahi sana kusikia kuwa eneo la ofisi ya MCDA lipo. Sambamba na hayo ameahidi kufanya harambee ambapo amewataka viongozi wa MCDA kuchangia pesa ili zipatikane tofali 400 ambazo ni sawa na chumba kimoja. Yeye atafanya harambee kwa wenyeviti, ambapo watatoa mfuko mmoja mmoja na  yeye atatoa mifuko miwili. Kama alivyofanya harambee shule ya mkoloni mpaka sasa madarasa kadhaa na ofisi vimekamilika na watoto wa chekechea wanaendelea namasomo yao. 



Imeandaliwa na Afisa Habari MCDA

Maoni